27
Vikosi Vya Jeshi
Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000.
 
Msimamizi wa kikosi cha kwanza kwa mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Kulikuwa na watu 24,000 katika kikosi chake. Yeye alikuwa mzao wa Peresi, na mkuu wa maafisa wote wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.
Msimamizi wa kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai Mwahohi. Miklothi ndiye alikuwa kiongozi wa kikosi chake. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000. Huyu ndiye yule Benaya aliyekuwa shujaa miongoni mwa wale Thelathini na ndiye alikuwa juu yao hao Thelathini. Mwanawe Amizabadi ndiye alikuwa mkuu katika kikosi chake.
Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Jemadari wa kikosi cha tano kwa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi Mwizrahi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Jemadari wa kikosi cha sita kwa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
10 Jemadari wa kikosi cha saba kwa mwezi wa saba alikuwa Helesi Mpeloni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
11 Jemadari wa nane kwa mwezi wa nane, alikuwa Sibekai Mhushathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
12 Jemadari wa tisa kwa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri Mwanathothi wa Wabenyamini. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
13 Jemadari wa kumi kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai Mnetofathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
14 Jemadari wa kumi na moja kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya Mpirathoni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
15 Jemadari wa kumi na mbili kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai Mnetofathi kutoka jamaa ya Othnieli. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Maafisa Wa Makabila
16 Maafisa waliokuwa wanaoongoza makabila ya Israeli walikuwa:
 
Kwa Wareubeni: Eliezeri mwana wa Zikri;
kwa Wasimeoni: Shefatia mwana wa Maaka;
17 kwa Walawi: Hashabia mwana wa Kemueli;
kwa Aroni: Sadoki;
18 kwa Yuda: Elihu, nduguye Daudi;
kwa Waisakari: Omri mwana wa Mikaeli;
19 kwa Wazabuloni: Ishmaya mwana wa Obadia;
kwa Wanaftali: Yeremothi mwana wa Azrieli;
20 kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia;
kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya;
21 kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria;
kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri;
22 kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu.
Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli.
 
23 Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Bwana alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani. 24 Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi.
Wasimamizi Wa Mali Za Mfalme
25 Azmawethi mwana wa Adieli ndiye alikuwa msimamizi wa hazina za mfalme.
Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia.
26 Ezri mwana wa Kelubu alikuwa msimamizi wa wafanyakazi waliolima katika mashamba.
27 Shimei Mramathi alikuwa msimamizi wa mashamba ya mizabibu.
Zabdi Mshifmi alikuwa msimamizi wa zabibu, utengenezaji na uhifadhi wa divai katika mapipa makubwa.
28 Baal-Hanani Mgederi ndiye alikuwa mwangalizi wa mashamba ya mfalme ya mizeituni na mikuyu katika tambarare za vilima vya magharibi.
Yoashi alikuwa msimamizi wa ghala za mafuta ya zeituni.
29 Shitrai Msharoni alikuwa msimamizi wa makundi ya ngʼombe waliojilisha huko Sharoni.
Shafati mwana wa Adlai alikuwa msimamizi wa yale makundi ya ngʼombe yaliyokuwa makondeni.
30 Obili Mwishmaeli alikuwa msimamizi wa ngamia.
Yedeya Mmeronothi alikuwa msimamizi wa punda.
31 Yazizi Mhagri alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi.
Hawa wote ndio waliokuwa maafisa wasimamizi wa mali alizokuwa nazo Mfalme Daudi.
 
32 Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme.
33 Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme.
Hushai Mwariki alikuwa rafiki wa mfalme. 34 Baada ya Ahithofeli, Yehoyada mwana wa Benaya aliingia mahali pake kama mshauri wa mfalme pamoja na Abiathari.
Yoabu alikuwa ndiye jemadari wa majeshi ya mfalme.